Fahamu aina mbalimbali za pochi kazi zake na umuhimu wake kwa wanawake

Pochi  ni  muhimu  sana katika maisha ya mwanamke yeyote.Pochi  utumika kila eneo la maisha kuanzia nyumbani ,kazini kanisani,n.k
Pochi zipo za aina mbalimbali kwa matumizi mbalimbali.Pochi uongeza umaridadi katika muonekano wa mwanamke hivyo ni muhimu kuangalia ubebeji wa pochi kulingana na mahali,tukio na hata ikiwezekena mavazi.

POCHI SAIZI YA KATI.

Pochi hii utumika katika shuguli mbalimbali za kila siku inafaa iwe na rangi itakayokuwezesha kuivaa na nguo nyingi  iwezekanavyo,mfano rangi nyeusi,dark brown,audark grey.Pochi hii aifai iwe na vikorombwezo vingi ,iwe tu plaini yenye muundo wa kuvutia na uwezo wa kubeba vitu muhimu vya kila siku kama waeti,simu ,diary,na vitu vingine vidogodogo.Pochi hii unaweza kwenda nayo kazini,kanisani,mkutanoni,n.k


POCHI YA SAIZI YA KUBWA


Inaweza kuwa ya ngozi au vinginevyo,kwa rangi yoyote unayoipenda na kwa aina yoyote ile.Pochi  hii utatumia kwenda nayo  shopping au matembezeni yoyote ambayo unajua utahitaji kuweka vitu vingi kwenye pochi ,kwa wale wenye watoto wadogo pochi hii inafaa sana maana itakuwezesha kubeba mahitaji yote ya mtoto kama diapers,maziwa,juice,nguo,nepi n.k.

POCHI YA MKONONI[clutch/Purse]

Pochi hii maalumu hasa unapotok usiku kwenda kwenye sherehe au chakula cha usiku.Zipo za aina na rangi tofauti na inapendeza zaidi kama ukimechi na rangi ya viatu au herein.Ni ochi ya kushiks mkononi na itakuwa na uwezo wa kuweka vitu vidogodogo kama simu,lipshiner,lipstick.

WALETI.

Hii ni pochi ndogo ambayo mara nyingi huwekwa ndani ya pochi kubwa na hubeba fedha,kadi mbalimbali,risiti na hata simi.Waleti zipo za aina  tofauti huweza pia kutumika yenyewe pale unapokuwa unaenda mahali ambapo huitaji kubeba vitu vingi zaidi vinavyokaa ndani ya wallet









0 maoni:

Angalia hapa picha za Mchumba wa Diamond Olatnumz Zari TheBoss Lady Mimba ilivyokua sasa Mambo hadharani

Siku za star kutokea Bongo Diamond platnumz anaetamba hivi sasa kwa nyimbo yake ntampata wapi kuitwa baba zinaendelea kuyoyoma Wiki mbili nyuma tetesi ziliibuka kuwa Mchumba wake Zari Theboss Lady kuwa mjamzito marafiki wa karibu wa star huyu wamerithibitisha hilo.







0 maoni:

MAAJABU YA DENCER WA BEYONCE NI MTOTO WA MIAKA MITATU !

angalia hapa VIDEO ya dancer wa msanii BEYONCE mdogo kuliko wote ana umri wa MIAKA MITATU tu! ANAITWA Heaven mambo yake ni hatari.

0 maoni:

Tottenham yafanya yao...

Harry Kane aliendelea kuimarika baada ya kuifunga Arsenal mabao mawili huku Tottenham ikitoka nyuma na kuibuka kidedea kwa mabao 2-1 katika mechi ya London Derby.

Kane alifunga baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Mousa Dembele aliyegusa krosi ya kona mapema katika kipindi cha pili.

Baadaye alifunga kichwa kizuri katika dakika ya 86 na kuiweka Spurs juu ya Gunners katika jedwali la ligi ya Uingereza .

Mesut Ozil aliiweka Arsenal kifua mbele katika kipindi cha kwanza laki mshambulizi yasio koma ya Tottenham katika ngome ya Arsenal yalizaa matunda na kuiweka Tottenham kuibuka kidedea.


0 maoni:

MAFUTA Yapungua bei zaidi TANZANIA

Mamlaka ya udhibiti wa Nishati ,Maji na mafuta EWURA nchini Tanzania imetangaza punguzo la jingine la mafuta nchini hali inayoleta matumaini tofauti,huku baadhi ya wananchi wakitaraji kunufaika kwa kupungua kwa gharama nyingine za huduma ya usafiri,lakini bado wamiliki wa mabasi ya masafa marefu wanasema punguzo hilo halina unafuu wowote kwao.

Afisa mahusiano wa EWURA nchini Tanzania Titus Kaguo amesema kuwa pamoja na punguzo hilo lakini ingeweza kupungua hadi kufikia chini ya dola moja yaani shilini 600 za kitanzania,lakini kiwango hicho hakijafikiwa kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi.

Akizungumzia utekelezaji wa amri ya mamlaka hiyo kwa wamiliki wa vituo vya mafuta kushusha bei,Kaguo amesema kuwa kwa sasa wanakusanya taarifa kutoka nchi nzima ili kubaini wanaokaidi amri hiyo.
Kwa upande wao wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani baadhi yao,wamesema kuwa punguzo hilo halina manufaa kwao kuwawezesha kushusha gharama za usafiri kwa kuwa gharama zingine za uendeshaji hazijapungua.
Yudika Mremi ni mmiliki wa kamupini ya mabasi ya Dar Express yaendayo mikoani,anasema kuwa gharama za uagizaji wa mabasi na vipuri bado kodi yake ipo juu.


0 maoni: