(PICHA) kwa mara ya kwanza Mbwana Samatta, Lionel Messi na Neymar kwenye Game ya FIFA 16 kwa pamoja

Kwa wale WATU WAZURI ambao ni wafwatiliaji na wapenzi wa michezo ya game hususani game za mchezo wa mpira wa miguu maarufu kama Play Station, huwa ni kawaida kuona wataalam wa game duniani kutengeneza game za timu zinazopendwa na muonekano wa wachezaji wa timu husika lengo likiwa kujenga taswira halisi kwa mchezaji wa game na kuongeza uvutiaji zaidi pindi unapo cheza game.

Kama ulikua hufahamu mtanzania Mbwana Samatta ambaye amejiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya huko  Jamuhuri ya Kongo kwa dau linalokadiliwa kuwa ni euro 800,000, ameingizwa katika ya Play Station ya FIFA 16

Hii ni habari nzuri kwa watu wa Tanzania kwani wataalamu wa mambo wanakwambia inasemekana Mbwana Samatta anaweza kuwa mchezaji wa mpira wa miguu wa kwanza kuwepo katika game hili la FIFA 16






,,,,Tuendelee kuiboresha familia ya #WATU #WAZURI for more info nifate instagram kwa @pascalzambwe

0 maoni:

"PIGO" Baada ya kumpoteza Banza Familia imempoteza tena mama na dada wa Banza Stone leo

"Inasikitisha" February 29 familia ya marehemu msanii wa muziki wa dansi Ramadhani Masanja maarufu kama Banza Stone imepata pigo tena tena ikiwa ni zaidi ya miezi minne imepita toka impoteze msanii huyo, familia ya Banza leo February 29 imeondokewa na watu wawili muhimu kwa Banza.

Leo zimeripotiwa taarifa za familia hiyo kupata misiba miwili ya watu muhimu kwa marehemu Banza Stone, kwa taarifa zilizotoka ni kuwa mama mzazi wa Banza Stone na dada yake wamefariki.

...Tuendelee kuiboresha familia ya WATU WAZURI for more info nifate instagram kwa @pascalzambwe


0 maoni:

"UTAFITI" Zika inasababisha kupooza

Utafiti mpya,umetoa ushahidi kuonyesha kwamba virusi vya Zika vinaweza kuathiri vibaya kinga ya mwili.Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu waliougua Zika miaka miwili iliyopita eneo moja la Ufaransa. Iligunduliwa baadhi ya wagonjwa walipooza na hata baadhi wakafariki dunia kutokana na maambukizi ya Zika.

Virusi hivyo ambavyo vimesambaa kwa kasi kanda ya Amerika Kusini vimelaumiwa kusababisha dosari za kimaumbile hasa ukuaji wa ubongo kwa watoto wanaozaliwa.
Utafiti mpya umechapishwa na jarida la afya la Lancet.

Virusi hivyo ambavyo vimesambaa kwa kasi kanda ya Amerika Kusini vimelaumiwa kusababisha dosari za kimaumbile hasa ukuaji wa ubongo kwa watoto wanaozaliwa.
Utafiti mpya umechapishwa na jarida la afya la Lancet.
 PICHA; Mtoto aliyeambukizwa Zika anazaliwa na kichwa kidogo.


...Tuendelee kuiboresha familia ya WATU WAZURI for more info nifollow instagram kwa @pascalzambwe


0 maoni:

Majambazi watatu wameuawa Arusha, na kuacha ujumbe kwa aliyekuwa kamanda wa Polisi Dar Suleiman Kova

Jeshi la Polisi Arusha limewaua majambazi watatu waliokuwa wakihusika na matukio ya wizi, pia liliwakuta wakiwa na milipuko ya bovu, bunduki, mavazi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) pamoja na ujumbe maalum kwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Dar es salaam, Suleiman Kova.
Ujumbe uliandikwa ‘Nasaha kwa Kova, Mzee andaa kamati ya mazishi ya vipolisi vyako tukiwamaliza tutakufikia wewe‘


Kamanda wa Polisi Arusha Liberatus Sabas amesema ‘Jeshi la Polisi Arusha lilipata taarifa kuwa kuna mtu wanamuhisi ni mharifu, tukaweka mtego na kumkamata mtu mmoja, tulipofanya msako katika chumba chake na kukuta milipuko kadhaa‘
‘Alieleza kuwa kuna wenzake anashirikiana nao katika matukio ya ujambazi,  usiku majira ya saa 5 Polisi wakiambatana na mtuhumiwa walifika eneo walipokuwa wenzake, baada ya kufika mtuhumiwa alipiga kelele na wenzake wakajua kwamba kuna matatizo ‘

Marushiano ya risasi yakaanza kufanyika na hatimaye Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi, jitihada za kuwapeleka hospitali zilishindwa kwasababu watu hao wote walifariki wakati wakipelekwa hospitali.

...tuendelee kuiboresha familia ya WATU WAZURI for more info nifollow instagram kwa @pascalzambwe

0 maoni: