(PICHA) kwa mara ya kwanza Mbwana Samatta, Lionel Messi na Neymar kwenye Game ya FIFA 16 kwa pamoja

0 maoni
Kwa wale WATU WAZURI ambao ni wafwatiliaji na wapenzi wa michezo ya game hususani game za mchezo wa mpira wa miguu maarufu kama Play Station, huwa ni kawaida kuona wataalam wa game duniani kutengeneza game za timu zinazopendwa na muonekano wa wachezaji wa timu husika lengo likiwa kujenga taswira halisi kwa mchezaji wa game na kuongeza uvutiaji zaidi pindi unapo cheza game.

Kama ulikua hufahamu mtanzania Mbwana Samatta ambaye amejiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya huko  Jamuhuri ya Kongo kwa dau linalokadiliwa kuwa ni euro 800,000, ameingizwa katika ya Play Station ya FIFA 16

Hii ni habari nzuri kwa watu wa Tanzania kwani wataalamu wa mambo wanakwambia inasemekana Mbwana Samatta anaweza kuwa mchezaji wa mpira wa miguu wa kwanza kuwepo katika game hili la FIFA 16






,,,,Tuendelee kuiboresha familia ya #WATU #WAZURI for more info nifate instagram kwa @pascalzambwe

"PIGO" Baada ya kumpoteza Banza Familia imempoteza tena mama na dada wa Banza Stone leo

0 maoni
"Inasikitisha" February 29 familia ya marehemu msanii wa muziki wa dansi Ramadhani Masanja maarufu kama Banza Stone imepata pigo tena tena ikiwa ni zaidi ya miezi minne imepita toka impoteze msanii huyo, familia ya Banza leo February 29 imeondokewa na watu wawili muhimu kwa Banza.

Leo zimeripotiwa taarifa za familia hiyo kupata misiba miwili ya watu muhimu kwa marehemu Banza Stone, kwa taarifa zilizotoka ni kuwa mama mzazi wa Banza Stone na dada yake wamefariki.

...Tuendelee kuiboresha familia ya WATU WAZURI for more info nifate instagram kwa @pascalzambwe


"UTAFITI" Zika inasababisha kupooza

0 maoni
Utafiti mpya,umetoa ushahidi kuonyesha kwamba virusi vya Zika vinaweza kuathiri vibaya kinga ya mwili.Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu waliougua Zika miaka miwili iliyopita eneo moja la Ufaransa. Iligunduliwa baadhi ya wagonjwa walipooza na hata baadhi wakafariki dunia kutokana na maambukizi ya Zika.

Virusi hivyo ambavyo vimesambaa kwa kasi kanda ya Amerika Kusini vimelaumiwa kusababisha dosari za kimaumbile hasa ukuaji wa ubongo kwa watoto wanaozaliwa.
Utafiti mpya umechapishwa na jarida la afya la Lancet.

Virusi hivyo ambavyo vimesambaa kwa kasi kanda ya Amerika Kusini vimelaumiwa kusababisha dosari za kimaumbile hasa ukuaji wa ubongo kwa watoto wanaozaliwa.
Utafiti mpya umechapishwa na jarida la afya la Lancet.
 PICHA; Mtoto aliyeambukizwa Zika anazaliwa na kichwa kidogo.


...Tuendelee kuiboresha familia ya WATU WAZURI for more info nifollow instagram kwa @pascalzambwe


Majambazi watatu wameuawa Arusha, na kuacha ujumbe kwa aliyekuwa kamanda wa Polisi Dar Suleiman Kova

0 maoni
Jeshi la Polisi Arusha limewaua majambazi watatu waliokuwa wakihusika na matukio ya wizi, pia liliwakuta wakiwa na milipuko ya bovu, bunduki, mavazi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) pamoja na ujumbe maalum kwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Dar es salaam, Suleiman Kova.
Ujumbe uliandikwa ‘Nasaha kwa Kova, Mzee andaa kamati ya mazishi ya vipolisi vyako tukiwamaliza tutakufikia wewe‘


Kamanda wa Polisi Arusha Liberatus Sabas amesema ‘Jeshi la Polisi Arusha lilipata taarifa kuwa kuna mtu wanamuhisi ni mharifu, tukaweka mtego na kumkamata mtu mmoja, tulipofanya msako katika chumba chake na kukuta milipuko kadhaa‘
‘Alieleza kuwa kuna wenzake anashirikiana nao katika matukio ya ujambazi,  usiku majira ya saa 5 Polisi wakiambatana na mtuhumiwa walifika eneo walipokuwa wenzake, baada ya kufika mtuhumiwa alipiga kelele na wenzake wakajua kwamba kuna matatizo ‘

‘Marushiano ya risasi yakaanza kufanyika na hatimaye Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi, jitihada za kuwapeleka hospitali zilishindwa kwasababu watu hao wote walifariki wakati wakipelekwa hospitali.

...tuendelee kuiboresha familia ya WATU WAZURI for more info nifollow instagram kwa @pascalzambwe

''Sanjay Dutt' Nyota wa Bollywood aachiliwa huru

0 maoni
Zimepita takribani siku tatu sasa tangu Nyota wa filamu za Bollywood Sanjay Dutt kuachiliwa kutoka jela katika mji wa magharibi wa Pune nchini India.

Dutt mwenye umri wa miaka 56 alihukumiwa kifungo jela kufuatia makosa ya kumiliki silaha inayohusishwa na mlipuko wa 1993 mjini Mumbai ambapo takriban watu 257 waliuawa na wengine 713 kujeruhiwa.
Alipatikana na hatia ya kununua silaha hiyo kutoka kwa walipuaji ,lakini akasema kwamba silaha hizo zilikuwa muhimu kwa lengo la kuilinda familia yake wakati wa ghasia za Waislamu dhidi ya Hindu.
Nyota huyo baadaye alipelekwa hadi katika jela ya Pune mwaka 2013 ili kukamilisha kipindi chake cha miaka mitrano.
Hatahivyo alipewa msahama wa siku 144 baada ya kuonekana kuwa na tabia njema na vitendo kama vile kusimamia kipindi cha redio


.......Tuendelee kuiboresha familia ya #WATU #WAZURI  For more info niffolow instagram kwa @pascalzambwe

Ndani ya siku 87 "HELLO'' Ya Adele yafanya miujiza youtube

0 maoni
Wimbo wa Adele umekuwa wimbo uliopendwa sana kwa muda mfupi sana kama ulikua hujui #MTU #MZURI wimbo huu wa adele unaambiwa ndio wimbo uliorudiwa kuimbwa mara nyingi na wasanii mbali mbali duniani kote.

lakini unajua kwamba rekodi zinaonesha wimbo huo una kama siku 88 tu hewani, hesabu ambayo kwa tafsiri nyingine ni miezi mitatu !!
Ninayo stori ambayo wameiandika pia kwenye page ya CNN mtandaoni kwamba wimbo wa ‘Hello‘ uliomrudisha Adele kwenye kilele cha kusikilizwa kwa mara nyingine, wimbo huo umetazamwa mara bilioni 1 kwenye channel ya Youtube.

Ngoma hiyo inakuwa ya 17 kuingia kwenye rekodi ya kutazamwa na watu zaidi ya bilioni 1 kwenye mtandao huo.Rekodi zinaonesha mwaka 2013 wimbo wa ‘Roar‘ staa wa Marekani, Katty Perry uliingia kwenye rekodi ya kutazamwa mara bilioni moja baada ya siku 487, mwaka 2014 kukawa na rekodi ya wimbo ‘Black Space‘ wa Taylor Swift uliingia rekodi ya kuangaliwa mara bilioni moja baada ya siku 238

Mwaka 2015 umekuwa mwaka wa Adele, wimbo ‘Hello‘ umeingia kwenye rekodi hiyo ndani ya siku 87, huenda ndio wimbo ambao umetazamwa na watu wengi zaidi ndani ya siku chache kwenye rekodi za Youtube
.....Tuendelee kuiboresha familia ya #WATU#WAZURI for more info nifate instagram kwa @pascalzambwe

kama hukupata nafasi #MTU #MZURI ya kuingia kwenye list ya watu walioutazama wimbo wa adele mara nyingi zaidi duniani, unaweza kuitazama hapa chini nimekuwekea #MTU #MZURI.
 





(VIDEO) Angalia hapa samaki wa ajabu na wanaovutia zaidi duniani

0 maoni
kama ulikua hujui #MTU#MZURI kuna Baadhi ya vitu vipo hapa duniani, vitu vinavutia zaidi kwa kuviangalia vipo dunia hii tunayoishi lakini hujawahi kupata nafasi ya kuviona, kuhusu hilo usijari kwani #MTU#MZURI nipo hapa kwaajiri yako nitahakikisha naku;letea vitu mbali mbali vinavovutia duniani  na hata unapoviangalia unajiskia furaha na kusema ''kweli mungu wa ajabu"

Leo #mtu #mzuri nimekuletea video ya samaki wanaovutia zaidi duniani wanapatikana chini kabisa ya kina cha bahari huku wakiwa na rangi nzuri na maumbo ya ajabu yanayo vutia zaidi 

nimekuwekea video hapa chini unaweza kuitazama na kuidownload



,,,,,,Tuendelee kuiboresha familia ya #WATU#WAZURI For more info nifollow instagram kwa @pascalzambwe