'AMUUA' mwanae kwa kumcoma moto

WEKA TANGAZO

Mwanamke nchini Marekani anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji baada ya kuamua kumweka mtoto wake aliyetoka kujifungua katikati ya barabara kisha kumchoma moto.

Mwendesha mashtaka aliyekua akisimamia kesi hiyo alisema mwanamke huyo Hyphernkemberly DORVILLIER anashtakiwa kwa kosa la kuua kwa kudhamilia.

Polisi walipofika eneo la tukio walimkuta mtoto huyo akiteketea kwa moto katikati ya barabara ya makazi ya watu ambayo ni maili 30 kutoka jiji la Mashariki mwa mji wa Philadelpia na kumkimbiza katika hospitali ya St. Christopher lakini alifariki masaa mawili baadae.

Baadhi mashahidi walithibitisha na kusema walimwona mwanamke huyo  akichoma kitu lakini hawakujua ni nini na walipomuuliza alisema alikuwa akichoma uchafu.

WEKA TANGAZO

0 maoni: