Messi: Siondoki Barcelona

WEKA TANGAZO
Pamoja na kuwepo kwa tetesi nyingi kuhusiana na mustakabali wa muda mrefu wa Lionel Messi baada ya kuwepo kwa mgogoro ndani ya klabu hiyo huku uhusiano wake na kocha Luis Enrique ukiwa mbaya imefahamika kuwa Lionel Messi hataondoka kwenye klabu hii.

Messi ambaye amecheza Barcelona tangu akiwa na umri wa miaka 13 amehusishwa na usajili wa kwenda Chelsea hasa baada ya kuonekana akiwa ame-follow ukurasa rasmi wa klabu hiyo kwenye mtandao wa Instagram.

Pamoja na kuwepo kwa nyakati tofauti hapo awali ambapo nyota huyo amekanusha vikali kuwa hawezi kuondoka Barcelona sababu ya msingi ya Messi kutoondoka imetajwa na ukiangalia kwa ndani utagundua kuwa ina mashiko kwa nyota huyo.
Messi alimuahidi marehemu Tito Vilanova kuwa hataihama Barcelona.
Messi alimuahidi marehemu Tito Vilanova kuwa hataihama Barcelona.
Imeelezwa kuwa Messi alimuahidi kocha wa zamani wa Barcelona hayati Tito Vilanova kuwa atacheza kwenye klabu hii mpaka mwisho wa muda wake wa kucheza soka na kama akihama basi itakuwa kurudi kwao Argentina na si kwenye klabu nyingine kubwa ya ulaya .
Ahadi hii Messi aliitoa kwa kocha huyu aliyefariki dunia mwaka jana wakati akiwa kwenye siku za mwisho za uhai wake na kama isingelikuwa hivyo basi huenda angekuwa tayari ameondoka .
Messi inaelezwa kuwa alikuwa mtu wa karibu sana wa hayati Ttito na alikuwa moja kati ya watu walioguswa sana na msiba wa kocha huyu wa zamani na kucheza kwake ndani ya Barcelona kwa sasa ni kwa ajili ya kocha huyo .
WEKA TANGAZO

0 maoni: