MATAJIRI Duniani Kumiliki mari zaidi ifikapo 2016... na sisi MASIKINI JE???
WEKA TANGAZO
Shirika la kimataifa la misaada
nchini Uingereza, Oxfam, limeonya kwamba kufikia mwaka ujao, matajiri
ambao ni asilimia moja ya idadi ya watu duniani, watamiliki mali zaidi
kuliko asilimia 99 iliyosalia ya watu.
Shirika hilo linataka
kuongeza shinikzo kwa wanasiasa kukabiliana na suala la ukosefu wa usawa
katika umiliki wa mali wakati viongozi wanajitayarisha kukutana nchini
Switzerland wiki hii kwa kongamano la uchumi duniani.Oxfam inasema kuna ongezeko kubwa la pengo kati ya utajiri na maskini.
Linasema
umewadia wakati kwa viongozi duniani kuwajibika zaidi. Mkuu wa masuala
ya nje wa shirika hilo, Katie Wright, amesema mojawapo ya mambo ambayo
yanastahili kukabiliwa ni ukwepaji wa kulipa kodi.
Kwa mujibu wa
shirika la Oxfam, mali ya matajiri walio wachache duniani iliongezeka
kwa asilimia 48 mwaka jana kutoka asilimia 44 mnamo mwaka 2009.
Kupanuka
kwa pengo kati ya maskini na matajiri duniani kumekuwa kizingiti katika
vita dhidi ya umaskini kwani makampuni makubwa zaidi duniani
yanashinikiza Marekani na Ulaya kushurutisha matajiri kulipa kodi kwani
watu wanaolipa sana kodi ni wale wenye kipato cha kadri.
''Je
tunataka kuishi katika dunia ambayo matajiri ambao ni asilimia 1
wanaomiliki mali nyingi kuliko watu wengi duniani?''alihoji afisaa mkuu
mtendaji wa Oxfam alisema katika taarifa yake, Winnie Byanyima,
''Kiwango
cha pengo kati ya maskini na matajiri duniani ni kubwa sana na licha ya
swala hilo kuangaziwa, pengo hilo bado linaendelea kupanuka.''
''Wakati
viongozi wa dunia kama vile Barack Obama na mkuu wa shirika la fedha
duniani Christine Lagarde wamezungumza swala la kupunguza umaskini
duniani, bado tunasubii viongozi watakaochukua hatua,''alisema Byanyima.
Taasisi
za afya na za kifedha, zilitumia mamilioni ya dola kuishinikiza
Marekani kuweka sheria nzuri mnamo mwaka 2013 na zaidi ya dola milioni
200 ilitumika jkusihinikiza Ulaya kubadilisha mambo.
Wakati
huohuo, mmoja kati ya watu 9 hawana chakula na watu zaidi ya bilioni
moja wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku, takwimu ambazo zinatoa
tasiwra mbaya sana kwa matajiiri duniani.
Shirika la Oxfam linatoa
wito kwa viongozi wa dunia kuhakikisha kwamba mashirka au kampuni za
watu matajiri zinalipa kodi huku serikali zikiongeza shinikizo
kuhakikisha kwamba watu maskini wanapata huduma za afya na elimu
WEKA TANGAZO
0 maoni: