Waasi 'waiteka' ikulu ya Rais Yemen
WEKA TANGAZO
Makabiliano makali yametokea kati ya
waasi wa kishia wa Houthi na vikosi vya usalama katika ikulu ya Rais
ambao inasadikiwa waasi hao wameiteka ikulu ya Rais.
Walioshuhudia
makabiliano hayo wanasema waasi hao walipambana na vikosi vya usalama
kwa muda kabla ya kuingia katika ikulu ya Rais.
Awali, Rais Abd
Rabbuh Mansour Hadi alifanya mazungumzo ya dharura na washauri wake siku
moja baada ya vifo vya watu tisa kufuatia makabiliano mengine kati ya
waasi hao na wanajeshi mnamo Jumatatu
Makabiliano makali yametokea kati ya
waasi wa kishia wa Houthi na vikosi vya usalama katika ikulu ya Rais
ambao inasadikiwa waasi hao wameiteka ikulu ya Rais.Walioshuhudia
makabiliano hayo wanasema waasi hao walipambana na vikosi vya usalama
kwa muda kabla ya kuingia katika ikulu ya Rais.
Awali, Rais Abd
Rabbuh Mansour Hadi alifanya mazungumzo ya dharura na washauri wake siku
moja baada ya vifo vya watu tisa kufuatia makabiliano mengine kati ya
waasi hao na wanajeshi mnamo Jumatatu.
Makubaliano yalifikiwa lakini waasi wa Houthis waliendelea kuzingira ikulu ya Rais na makao ya waziri mkuu.
Kiongozi
wa waasi hao anatarajiwa kutoa hotuba baadaye leo wakati baraza la
usalama la Umoja wa Mataifa likijiandaa kwa mkutano wa dharura kujadili
hali nchini Yemen.
Kanali Saleh al-Jamalani, ambaye ni mkuu wa
kikosi cha ulinzi wa ikulu ya Rais Abed Rabbo Mansour Hadi, ameambia
shrika la habari la AP kwamba waasi haowalivamia ikulu nyakati za
mchana.Rais Hadi inaarufiwa hakuwa katika makao hayo wakati waasi walioivamia ikulu.
WEKA TANGAZO
0 maoni: