Fahamu aina mbalimbali za pochi kazi zake na umuhimu wake kwa wanawake

Pochi  ni  muhimu  sana katika maisha ya mwanamke yeyote.Pochi  utumika kila eneo la maisha kuanzia nyumbani ,kazini kanisani,n.k
Pochi zipo za aina mbalimbali kwa matumizi mbalimbali.Pochi uongeza umaridadi katika muonekano wa mwanamke hivyo ni muhimu kuangalia ubebeji wa pochi kulingana na mahali,tukio na hata ikiwezekena mavazi.

POCHI SAIZI YA KATI.

Pochi hii utumika katika shuguli mbalimbali za kila siku inafaa iwe na rangi itakayokuwezesha kuivaa na nguo nyingi  iwezekanavyo,mfano rangi nyeusi,dark brown,audark grey.Pochi hii aifai iwe na vikorombwezo vingi ,iwe tu plaini yenye muundo wa kuvutia na uwezo wa kubeba vitu muhimu vya kila siku kama waeti,simu ,diary,na vitu vingine vidogodogo.Pochi hii unaweza kwenda nayo kazini,kanisani,mkutanoni,n.k


POCHI YA SAIZI YA KUBWA


Inaweza kuwa ya ngozi au vinginevyo,kwa rangi yoyote unayoipenda na kwa aina yoyote ile.Pochi  hii utatumia kwenda nayo  shopping au matembezeni yoyote ambayo unajua utahitaji kuweka vitu vingi kwenye pochi ,kwa wale wenye watoto wadogo pochi hii inafaa sana maana itakuwezesha kubeba mahitaji yote ya mtoto kama diapers,maziwa,juice,nguo,nepi n.k.

POCHI YA MKONONI[clutch/Purse]

Pochi hii maalumu hasa unapotok usiku kwenda kwenye sherehe au chakula cha usiku.Zipo za aina na rangi tofauti na inapendeza zaidi kama ukimechi na rangi ya viatu au herein.Ni ochi ya kushiks mkononi na itakuwa na uwezo wa kuweka vitu vidogodogo kama simu,lipshiner,lipstick.

WALETI.

Hii ni pochi ndogo ambayo mara nyingi huwekwa ndani ya pochi kubwa na hubeba fedha,kadi mbalimbali,risiti na hata simi.Waleti zipo za aina  tofauti huweza pia kutumika yenyewe pale unapokuwa unaenda mahali ambapo huitaji kubeba vitu vingi zaidi vinavyokaa ndani ya wallet









0 maoni:

Angalia hapa picha za Mchumba wa Diamond Olatnumz Zari TheBoss Lady Mimba ilivyokua sasa Mambo hadharani

Siku za star kutokea Bongo Diamond platnumz anaetamba hivi sasa kwa nyimbo yake ntampata wapi kuitwa baba zinaendelea kuyoyoma Wiki mbili nyuma tetesi ziliibuka kuwa Mchumba wake Zari Theboss Lady kuwa mjamzito marafiki wa karibu wa star huyu wamerithibitisha hilo.







0 maoni:

MAAJABU YA DENCER WA BEYONCE NI MTOTO WA MIAKA MITATU !

angalia hapa VIDEO ya dancer wa msanii BEYONCE mdogo kuliko wote ana umri wa MIAKA MITATU tu! ANAITWA Heaven mambo yake ni hatari.

0 maoni:

Tottenham yafanya yao...

Harry Kane aliendelea kuimarika baada ya kuifunga Arsenal mabao mawili huku Tottenham ikitoka nyuma na kuibuka kidedea kwa mabao 2-1 katika mechi ya London Derby.

Kane alifunga baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Mousa Dembele aliyegusa krosi ya kona mapema katika kipindi cha pili.

Baadaye alifunga kichwa kizuri katika dakika ya 86 na kuiweka Spurs juu ya Gunners katika jedwali la ligi ya Uingereza .

Mesut Ozil aliiweka Arsenal kifua mbele katika kipindi cha kwanza laki mshambulizi yasio koma ya Tottenham katika ngome ya Arsenal yalizaa matunda na kuiweka Tottenham kuibuka kidedea.


0 maoni:

MAFUTA Yapungua bei zaidi TANZANIA

Mamlaka ya udhibiti wa Nishati ,Maji na mafuta EWURA nchini Tanzania imetangaza punguzo la jingine la mafuta nchini hali inayoleta matumaini tofauti,huku baadhi ya wananchi wakitaraji kunufaika kwa kupungua kwa gharama nyingine za huduma ya usafiri,lakini bado wamiliki wa mabasi ya masafa marefu wanasema punguzo hilo halina unafuu wowote kwao.

Afisa mahusiano wa EWURA nchini Tanzania Titus Kaguo amesema kuwa pamoja na punguzo hilo lakini ingeweza kupungua hadi kufikia chini ya dola moja yaani shilini 600 za kitanzania,lakini kiwango hicho hakijafikiwa kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi.

Akizungumzia utekelezaji wa amri ya mamlaka hiyo kwa wamiliki wa vituo vya mafuta kushusha bei,Kaguo amesema kuwa kwa sasa wanakusanya taarifa kutoka nchi nzima ili kubaini wanaokaidi amri hiyo.
Kwa upande wao wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani baadhi yao,wamesema kuwa punguzo hilo halina manufaa kwao kuwawezesha kushusha gharama za usafiri kwa kuwa gharama zingine za uendeshaji hazijapungua.
Yudika Mremi ni mmiliki wa kamupini ya mabasi ya Dar Express yaendayo mikoani,anasema kuwa gharama za uagizaji wa mabasi na vipuri bado kodi yake ipo juu.


0 maoni:

Mfaamu chatu wa kifilipino anayefanya massage(masaji)



article-0-1E0F9D0400000578-296_634x356 wageni wengi wanaotembelea bustani ya Cebu Zoo, Ufilipino moja ya vitu ambavyo wanafurahia ni hii ya huduma ya kufanyiwa massage na nyoka aina ya chatu.
Nyoka wanaofanya hii wako wanne, wamepewa majina kabisa, wanaitwa MichelleWalter,EJ na Daniel.
Wakati ilipoanzishwa ilikuwa ni huduma ya bure, lakini kwa sasa ni biashara, chatu hao wanahitaji kula kuku kumi kila mmoja kabla ya zoezi la massage kuanza.
Msimamizi wa bustani ya wanyama ambapo inatolewa huduma hiyo, Giovanni Romarate amesema wakati wanaanza biashara hiyo wageni walikuwa wanaogopa, lakini wengi waliojaribu waliipenda na sasa  hutolewa kwa kulipia, kila kinachopatikana kinatumika kuboresha bustani hiyo.
article-0-1E0F9D1D00000578-840_634x356
Python-Massage (1)
Pythons-Massage
article-0-1E0F9C4300000578-214_634x356
article-0-1E0F9D0400000578-296_634x356
deadly-python-massages-are-somehow-a-real-thing
imgsfubo
Snake massage at Cebu City Zoo


0 maoni:

Waasi 'waiteka' ikulu ya Rais Yemen

Makabiliano makali yametokea kati ya waasi wa kishia wa Houthi na vikosi vya usalama katika ikulu ya Rais ambao inasadikiwa waasi hao wameiteka ikulu ya Rais.

Walioshuhudia makabiliano hayo wanasema waasi hao walipambana na vikosi vya usalama kwa muda kabla ya kuingia katika ikulu ya Rais.

Awali, Rais Abd Rabbuh Mansour Hadi alifanya mazungumzo ya dharura na washauri wake siku moja baada ya vifo vya watu tisa kufuatia makabiliano mengine kati ya waasi hao na wanajeshi mnamo Jumatatu

 Makabiliano makali yametokea kati ya waasi wa kishia wa Houthi na vikosi vya usalama katika ikulu ya Rais ambao inasadikiwa waasi hao wameiteka ikulu ya Rais.Walioshuhudia makabiliano hayo wanasema waasi hao walipambana na vikosi vya usalama kwa muda kabla ya kuingia katika ikulu ya Rais.

Awali, Rais Abd Rabbuh Mansour Hadi alifanya mazungumzo ya dharura na washauri wake siku moja baada ya vifo vya watu tisa kufuatia makabiliano mengine kati ya waasi hao na wanajeshi mnamo Jumatatu.

Makubaliano yalifikiwa lakini waasi wa Houthis waliendelea kuzingira ikulu ya Rais na makao ya waziri mkuu.
Kiongozi wa waasi hao anatarajiwa kutoa hotuba baadaye leo wakati baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likijiandaa kwa mkutano wa dharura kujadili hali nchini Yemen.

Kanali Saleh al-Jamalani, ambaye ni mkuu wa kikosi cha ulinzi wa ikulu ya Rais Abed Rabbo Mansour Hadi, ameambia shrika la habari la AP kwamba waasi haowalivamia ikulu nyakati za mchana.Rais Hadi inaarufiwa hakuwa katika makao hayo wakati waasi walioivamia ikulu.


0 maoni:

WANASWA WAKIFANYA MAPENZI YA JINSIA MOJA

DUNIA imekwisha! Wasichana wawili warembo, Maua Sadick (24), mkazi wa Stakishari, Ukonga wilayani Ilala na Lucy Fred (23), mkazi wa Karakata jijini Dar es Salaam, wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga, Dar kwa kesi yenye jalada STK/RB/463/2015  wakidaiwa kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Warembo, Maua Sadick (mwenye shati la draft) na Lucy Fred wakipozi kimahaba.
Warembo hao walikamatwa Januari 12, mwaka huu saa sita mchana, nyumbani kwa Maua wakidaiwa kufanya ngono kinyume cha sheria ya kujamiiana ambapo watu wa jinsia moja ni makosa kukutana kimwili.
NDUGU, MAJIRANI WAKERWA
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, kukamatwa kwa Maua kulitokana na taarifa za baadhi ya ndugu na majirani zilizopelekwa polisi kwamba, wasichana hao wanapokuwa kwenye tendo la ndoa wamekuwa wakipiga kelele za udhalilishaji kwa familia zao.
Wasichana hao wakiwa maeneo tofauti.
WALISHAONYWA, HAWAKUSIKIA
Vyanzo makini kutoka jirani na makazi ya Maua vinadai kuwa, kutokana na hali hiyo, baadhi ya watu walijitolea kuwaonya wasichana hao kuwa na staha wawapo kwenye faragha yao lakini pia wao ni wanawake haiwezekani wacheze mchezo huo wenyewe kwa wenyewe lakini hawakutaka kusikia.
MAJIRANI WAFUNGULIA REDIO SAUTI YA JUU
“Ilifika mahali wakiingia chumbani kuanza mambo yao sisi majirani tunazidisha sauti za redio ili watoto wasisikie lakini na wao sauti zao zinakuwa juu kushinda za redio,” alisema jirani mmoja akiomba jina lake lifichwe ili kukwepa uhasama.
Alisema kutokana na hali hiyo waliamua kufikisha habari hizo polisi kwani ni kinyume cha sheria watu wa jinsia mmoja kukutana kimapenzi.
Mrembo Lucy Fred ambaye ni mpenzi wa Maua Sadick.
HISTORIA YA LUCY
Wakizidi kuzungumza na Uwazi, majirani hao walisema, Lucy ambaye ndiye anaitwa mke na Maua amekuwa akitoka nyumbani kwa wazazi wake Karakata kwa lengo la kumfuata Maua.
SIKU YA TUKIO
Ilisemekana kuwa, siku ya tukio, majirani walipoanza kusikia ‘zile sauti zao’, waliwapa polisi namba ya simu ya mtu wa jirani na Maua kwa lengo la kusaidia kufika nyumbani hapo.
“Polisi walipofika waligonga mlango kwa muda mrefu bila kufunguliwa na kelele za mahaba zilizidi kusikika.  Baadaye, nadhani wakati wanapumzika sasa, Maua alifungua mlango mkubwa na kukutana na macho ya polisi, wakambana na kumtaka waende wote alipo Lucy, wakaenda chumbani na kumkuta.
“Pia polisi walikuta kidude ambacho huwashwa kwa betri kilichodaiwa pia hutumika wakati wa tendo,” kilisema chanzo.
Warembo hao kama wanavyoonekana kwenye picha zao za instagram.
HISTORIA YA MAUA
Maua ni binti ambaye ni yatima, amekuwa akiishi mwenyewe kwenye nyumba hiyo kubwa ya familia  hivyo kumwita Lucy mara kwa mara kwa madai ya kufanya ufuska huo kwa vile wana uhuru.
Inasemekana kuwa, Maua siku zote amekuwa akivaa mavazi ya kiume licha ya kwamba, ni mwanamke kamili.
POLISI WASHANGAA
Taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya jeshi la polisi zinadai kwamba, hata wakiwa mahabusu ya kituo hicho, wawili  hao wamekuwa wakioneshana mapenzi baina yao kitendo kilichowashangaza mahabusu wengine na polisi pia.
Uwazi lilifika nyumbani kwa Maua na kukutana na mdogo wake aitwaye Aziz ambaye alikiri kukamatwa kwa Maua na kwamba tangu akamatwe hajarudi na wala hajui kinachoendelea huku akisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa sababu ya kutupiwa lawama na wanandugu kwamba yeye ndiye aliyepeleka taarifa polisi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki.
“Mimi sikai hapa, nimefika hivi karibuni nikitokea mkoani. Ndugu wananituhumu mimi kuita polisi, sijui mtu aliyewapa askari namba yangu wakanipigia kama  wageni wanaokuja nyumbani, nikawapa ramani na walipofika ndipo nikagundua ni askari,” alisema Aziz.
Mwenyekiti wa  Serikali ya Mtaa, George Mtambalike alipohojiwa na gazeti hili ofisini kwake alithibitisha kukamatwa kwa wasichana hao kwa madai ya kufanya mapenzi ya jinsia moja na aliwatembelea Kituo cha Polisi cha Stakishari.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alikiri kukamatwa kwao na akasema uchunguzi unaendelea.

0 maoni:

MATAJIRI Duniani Kumiliki mari zaidi ifikapo 2016... na sisi MASIKINI JE???

Shirika la kimataifa la misaada nchini Uingereza, Oxfam, limeonya kwamba kufikia mwaka ujao, matajiri ambao ni asilimia moja ya idadi ya watu duniani, watamiliki mali zaidi kuliko asilimia 99 iliyosalia ya watu.

Shirika hilo linataka kuongeza shinikzo kwa wanasiasa kukabiliana na suala la ukosefu wa usawa katika umiliki wa mali wakati viongozi wanajitayarisha kukutana nchini Switzerland wiki hii kwa kongamano la uchumi duniani.Oxfam inasema kuna ongezeko kubwa la pengo kati ya utajiri na maskini.
Linasema umewadia wakati kwa viongozi duniani kuwajibika zaidi. Mkuu wa masuala ya nje wa shirika hilo, Katie Wright, amesema mojawapo ya mambo ambayo yanastahili kukabiliwa ni ukwepaji wa kulipa kodi.

Kwa mujibu wa shirika la Oxfam, mali ya matajiri walio wachache duniani iliongezeka kwa asilimia 48 mwaka jana kutoka asilimia 44 mnamo mwaka 2009.

Kupanuka kwa pengo kati ya maskini na matajiri duniani kumekuwa kizingiti katika vita dhidi ya umaskini kwani makampuni makubwa zaidi duniani yanashinikiza Marekani na Ulaya kushurutisha matajiri kulipa kodi kwani watu wanaolipa sana kodi ni wale wenye kipato cha kadri.

''Je tunataka kuishi katika dunia ambayo matajiri ambao ni asilimia 1 wanaomiliki mali nyingi kuliko watu wengi duniani?''alihoji afisaa mkuu mtendaji wa Oxfam alisema katika taarifa yake, Winnie Byanyima,

''Kiwango cha pengo kati ya maskini na matajiri duniani ni kubwa sana na licha ya swala hilo kuangaziwa, pengo hilo bado linaendelea kupanuka.''

''Wakati viongozi wa dunia kama vile Barack Obama na mkuu wa shirika la fedha duniani Christine Lagarde wamezungumza swala la kupunguza umaskini duniani, bado tunasubii viongozi watakaochukua hatua,''alisema Byanyima.

Taasisi za afya na za kifedha, zilitumia mamilioni ya dola kuishinikiza Marekani kuweka sheria nzuri mnamo mwaka 2013 na zaidi ya dola milioni 200 ilitumika jkusihinikiza Ulaya kubadilisha mambo.

Wakati huohuo, mmoja kati ya watu 9 hawana chakula na watu zaidi ya bilioni moja wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku, takwimu ambazo zinatoa tasiwra mbaya sana kwa matajiiri duniani.

Shirika la Oxfam linatoa wito kwa viongozi wa dunia kuhakikisha kwamba mashirka au kampuni za watu matajiri zinalipa kodi huku serikali zikiongeza shinikizo kuhakikisha kwamba watu maskini wanapata huduma za afya na elimu


0 maoni:

'AMUUA' mwanae kwa kumcoma moto

Mwanamke nchini Marekani anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji baada ya kuamua kumweka mtoto wake aliyetoka kujifungua katikati ya barabara kisha kumchoma moto.

Mwendesha mashtaka aliyekua akisimamia kesi hiyo alisema mwanamke huyo Hyphernkemberly DORVILLIER anashtakiwa kwa kosa la kuua kwa kudhamilia.

Polisi walipofika eneo la tukio walimkuta mtoto huyo akiteketea kwa moto katikati ya barabara ya makazi ya watu ambayo ni maili 30 kutoka jiji la Mashariki mwa mji wa Philadelpia na kumkimbiza katika hospitali ya St. Christopher lakini alifariki masaa mawili baadae.

Baadhi mashahidi walithibitisha na kusema walimwona mwanamke huyo  akichoma kitu lakini hawakujua ni nini na walipomuuliza alisema alikuwa akichoma uchafu.


0 maoni:

Urembo bandia nusura unisababishie mauti


Mwanamke aliyemaliza katika nafasi ya pili ya mashindano ya urembo amesema kupenda sana kujiweka urembo bandia nusura umletee mauti yake.
Andressa Urach alimaliza wa pili katika  ya urembo ambapo mashabiki walimpigia mwanamke waliyehisi kuwa na makalio mazuri zaidi katika nchi yao kupitia kwenye mtandao wa internet.
Ili kujiongeza urembo, Urach aliambia jarida la Daily Mail la Uingereza kwamba alidungwa sindano za kemikali ili kufanya makalio yake kuwa makubwa pamoja na kuongeza ukubwa wa miguu yake.
Lakini mnamo mwaka 2013, mwili wake ulianza kuoza ndani.
Athari za kujiweka urembo bandia zilianza kumwandama wakati Urachhadi madaktari wakalazimika kutoa kemikali hizo kutoka mwilini mwake mwezi Novemba kwa kuchimba mashimo katika mapaja yake.

Mwili wake ilipatwa na mshtuko kwa sababu ya ugonjwa alioupata kwa kutumia vifaa vichafu vya matibabu mwilini mwake
Daktari mmoja wa kurekebisha na kutibu athari zinazotokana na urembo bandia alisema ugonjwa aliopuata Urach ulitokana vifaa vichafu.
Madaktari hata hivyo waliweza kuokoa maisha yake lakini hadi leo anatumia tu kiti cha magurudumu na miguu yake ina mashimo mwengi ambayo madaktari waliweza kutoboa ili kutoa kemikali zenye sumu alizotumia kuongeza ukubwa wa makalio na miguu.
''Ninalipia makosa yangu leo kwa sababu nilitaka urembo kwa kila hali, ili nionekane kuwa kamili. Mungu ananiadhibu'' Urach alisema.
''Lakini badala ya kujiongeza urembo, niliharibu mwili wangu na sasa hata hauna sura.
Urach pia alisema kwamba alikuwa na mazoea mabaya ya kufanyiwa uapasuaji wa kujiongeza urembo bandia kila alipojihisi kufanya hivyo.
''Sikuwahi kutafakari mara mbili wakati nilipokuwa nafanyiwa upasuaji lakini watu waliponionya nilidhani tu nitaweza kukabiliana na athari za hayo baadaye. '' Ningeweza kwenda kwa daktari, kama mfano nilivyozoea kwenda dukani na kuchagua nilichokitaka. Nilitaka watu wanitazame na kusema tu , ''wow''
Kwa sasa Urach amejitwika mzigo wa kuwatahadharisha wanawake wengine kuhusu hatari za urembo bandia
wabongo kazi kweu..........



0 maoni:

UNAMKUMBUKA...?? Mtoto aliyezaliwa na viungo nane juu ya tumbo lake...?


mwaka 2010 kijana huyu wa kihindi ambaye alizaliwa na viungo nane na kuheshimiwa kama Mungu alifanyiwa operesheni kumpa nafasi katika maisha ya kawaida. Deepak Paswan 7',Alizaliwa na pacha vimelea nje ya tumbo lake akiwa na miguu minne pamoja na mikono minne.


Read More »

0 maoni:

kutoka Shirikisho la soka dunia Fifa limetangaza kikosi cha wachezaji bora wa dunia

Kikosi hicho kinawajumuisha nyota watatu waliokua wakiwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia ambao ni Ronaldo,Messi na Neuer.
Kikosi kamili kipa ni Manuel Neuer. Mabeki Philipp Lahm, David Luiz, Thiago Silva na Sergio Ramos
Viungo Andres Iniesta, Toni Kroos, Angel di Maria.Huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Arjen Robben, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

0 maoni:

JUSTIN BIEBER ''Nitamfikisha mahakamani '' CALVIN KLEIN'

Kutoka NEW YOURK marekani msanii justin bieber amekasirishwa na picha iliyosambazwa mitaondoni inayomuonyesha akiwa na mwili mkubwa uliojaa huku akiwa amevaa boksa maarufu za mwanamitindo aneye faamika kwajina la calvin klein.


Read More »

0 maoni:

 msanii anaetamba kwa ngoma ya ''waalade'' Barnaba Boy leo ameachia ngoma yake mpya inayoitwa Mipango aliyomshirikisha mzee wa ''pesa' Mr Blue' maalum kwa ajili ya siku ya wapendanao na wanandoa Duniani, February  14 ambayo ipo kwenye album yake anayotarajia kuiachia mwezi April mwaka huu kaa tayari mtu mzuri kwani utaweza ku download hapa hapa.http://watuwazurii.blogspot.com/... #kwa #watu #wazuri


Read More »

0 maoni:

Kifahamu kisiwa cha ajabu kuliko vyote Duniani


1 maoni:

JE! Unawajua samaki wa ajabu na wanaovutia zaidi duniani?







0 maoni:

Wahanga wa shambulio la Ugaidi wakumbukwa Ufaransa

katika kanisa katoliki la Notre Dame mjini Paris, wakati raia wa Ufaransa walipowakumbuka wahanga wa shambulizi la kigaidi katika ofisi ya jarida la Ckatika kanisa katoliki la Notre Dame mjini Paris, wakati raia wa Ufaransa walipowakumbuka wahanga wa shambulizi la kigaidi katika ofisi ya jarida la Charlie Hebdo harlie Hebdo 

Raia waliokuwa katika eneo hilo waliweka kalamu, kuwasha mishuma na hata vijikaratasi vilivyokuwa na ujumbe wa huzuni na kulaani kitendo hicho. Mwanamke mmoja alisema kwa sauti “Mshikamano na Uhuru” huku akibubujikwa na machozi. Na ilipofika saa sita juu ya alama hivi ndivyo hali ilivyokuwa nchini Ufaransa.
Wafaransa walinyamaza kwa dakika moja kuwakumbuka wahanga wa shambulio hilo la kigaidi. Baadaye raia hao waliimba wimbo wa taifa, huku wakilia, wengi wakiwa na kalamu na penseli ishara ya wachora vibonzo waliolengwa katika shambulio hilo.


0 maoni:

Official Video | Nay Wa Mitego - Akadumba | watch&download


Read More »

0 maoni:

Messi: Siondoki Barcelona

Pamoja na kuwepo kwa tetesi nyingi kuhusiana na mustakabali wa muda mrefu wa Lionel Messi baada ya kuwepo kwa mgogoro ndani ya klabu hiyo huku uhusiano wake na kocha Luis Enrique ukiwa mbaya imefahamika kuwa Lionel Messi hataondoka kwenye klabu hii.

Read More »

0 maoni:

chege na Temba-kaunyika new mp3song

 single mpya ya wasanii kutokea tmk Wanaume Family, Chege na Temba inayoitwa kaunyika waliyomshirikisha Dj Maphorisa kutoka Afrika Kusini isikilize na ku download hapa


0 maoni: